Mabingwa wa Ufaransa PSG wamefanya mazungumzo na Juventus kuhusu uhamisho wa dau la £73m kumsajili mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 Paulo Dybala. (Mail)
Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho amewasili nchini Ujerumani ili kukamilisha mkopo wake wa msimu huu kwa mabingwa wa ujerumani Bayern Munich. (Sun)
Paris St-Germain wamemtaka beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 26, pamoja na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Junior, 19, katika mpango wa kubadilishana wachezaji iwapo wanamuitaji mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Neymar. (Telefoot - in French)
Barcelona inatumai kumrudisha Neymar Nou Camp , lakini kukiwa na kifungu cha kumnunua.. (Sport - in Spanish)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 34, anakaribia kujiunga na klabu ya Itali Lazio. Inter Milan, Fiorentina na Napoli pia zina hamu ya kumsaini raia huyo wa Uhispania , ambaye kwa sasa hana klabu. (Corriere Dello Sport - in Italian)
Inter Milan wanataka kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Chile Alexis Sanchez, 30, na pia wana hamu na mshambuliaji Llorente na kiungo wa kati wa Barcelona na raia wa Chile Arturo Vidal, 32. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Ajenti wa Sanchez yuko nchini Uingereza kuzungumzia mkopo wake kuelekea Inter Milan. (Sky Italy, via Sky Sports)
Sanchez alikua akifanya mazoezi na United siku ya Jumapili alfajiri.. (The Sun)
Inter Milan inajaribu kuafikia makubaliano ya kumnunua Sanchez lakini United imelazimika kumtoa kwa mkopo ili kutolipa mshahara wake wa £500,000 kwa wiki. (Mirror)
Manchester United wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi beki Eric Bailey mchezaji mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ivory Coast . (Sun)
Paris St-Germain na Bayern Munich huenda zikawasilisha ombi kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can, 25, baada ya kuambiwa na mkufunzi wake Maurizio Sarri anahitajiki Juventus. (Tuttosport, via Mail)
Paris St-Germain na Monaco zinafikiria kumpatia ofa kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 25, kwa kuwa muda wake Chelsea unaonekana kwamba umekwisha.. (Daily Express)
Celtic imeipatia ofa Bordeaux kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Olivier Ntcham . (20 Minutes via Daily Record)
Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce yuko tayari kumrudisha uwanjani mshambuliaji wa England Dwight Gayle, 28, haraka iwezekanavyo. (Newcastle Chronicle)
0 maoni:
0758057161