Homepage
» Tetesi za soka Ulaya Jumanne 31.07.2018: Willian, Courtois, Maguire, Rojo, Ramsey, Kante
Tetesi za soka Ulaya Jumanne 31.07.2018: Willian, Courtois, Maguire, Rojo, Ramsey, Kante
Posted at July 31, 2018 |  in
Image caption
Real Madrid wanasema hawamtaki mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian
Real Madrid haina
mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye
umri wa miaka 29, na wanaemtaka tu ni mlinda lango wa Ubelgiji
Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, kutoka the Blues. (marca)
Image caption
Mchezaji wa safu ya ulinzi Harry Maguire atasalia the Foxes katika msimu mpya
Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Willian anasema ni
mwenye ''furaha sana katika Chelsea na anafurahia kuishi London. (Globo
Esporte, via Mirror)
Meneja wa Leicester Claude Puel amesisitizia tena imani yake
kwamba mlinzi wa England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25 -
anayechezea Manchester United - atasalia na the Foxes katika msimu
mpya. (Sky Sports)
Maguire anatarajiwa kupewa donge nono katika
mkataba wake mpya na Leicester na hivyo kuongezewa malipo yake ya wiki
kutoka £50,000 hadi £95,000. (Mirror)
Image caption
Liverpool wanasema wanajiamini kuwa watamchukua Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane
Everton wako mstari wa mbele katika harakati za
kusaini mkataba na Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester United
na Argentina Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 28 ambae aliambiwa
anaweza kuondoka kama tahamani yake ya £30m itatimizwa. (Mirror)
Liverpool
wanajiamini kuwa wao ndio watakao saini mkataba na mshambuliaji wa
Senegal Sadio Mane, mwenye umri wa miaka 26, kwa mkataba wa muda mrefu
mnamo wiki zijazo. (Mirror)
Wakati huo huo , mchezaji wa the
Reds kutoka Ubelgiji Divock Origi, 23, anasakwa kwa deni na Besiktas
pamoja na Fenerbahce.(Talksport)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
The Blues wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji
wa kiungo cha kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey
Chelsea wamekuwa na mazungumzo ya wazi na Inter
Milan juu ya mchezaji wao wa safu ya kati , raia wa Uruguay Matias
Vecino, mwenye umri wa miaka 26, na wakatoa £35.5m kwa Juventus ili
wamchukue Muitaliano Mattia Caldara mwenye umri wa miaka anayecheza
safu ya ulinzi katika timu ya taifa ya Italia. (London Evening Standard)
The
Blues pia wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji wa kiungo cha
kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey, mweney umri wa miaka 27 kwa
£30m (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anasema lengo lake
kuu ni kumpata mshambuliaji wa Buyern Munich Robert Lewandowski,
Lazio
amembiwa na the Gunners kuwa lazima walipe £7m ikiwa wanataka
kusaini mkatapa na mchezaji wa safu ya mashambulizi Muhispania Lucas
Perez. (Talksport)
Newcastle wana nia ya kumchukua Nicolas
Tagliafico wa Ajax na mchezaji wa kimataifa wa Argentina , lakini
gharama ya £8m na madai ya mchezaji huyo wa safu ya nyuma kushoto
mwenye umri wa miaka 23 huenda yakawa zaidi ya bajeti iliyopo ya meneja
wa Magpies Rafael Benitez. (Newcastle Chronicle)
Image caption
Leicester imesema itakubali malipo ya £18m kumnunua mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemtaja mchezaji
wa Bayern Munich na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye
umri wa miaka 29, kuwa ndiye mchezaji anayemlenga zaidi kumnunua (Star)
Brighton imekubali kumuuza mshambuliaji wa England Sam Baldock mwenye umri wa miaka 29- kwa Reading. (Argus)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Mourinho amewasihi wachezaji kama Paul Pogba, Romelu
Lukaku na Jesse Lingard wapunguze mapumziko yao wawasaidie wachezaji
kwenye timu zao wasio na uwezo
Leicester itakubali malipo ya £18m kumnunua
mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, lakini hatma ya siku zijazo
ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 haijaamliwa mpaka mwishoni mwa
Agosti wakati msimu wa uhamisho utakapomalizi (Leicester Mercury)
Meneja
wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amekataa kuingizwa kwenye taarifa za
uvumi zinazokihusisha kilabu na uhamisho wa mchezaji wa Chelsea na
ttimu ya Ufaransa wa safu ya kati N'Golo Kante, mwenye umri wa miaka
27. (Talksport)
Image caption
Patrick Bamford anajiandaa kuhamia Leeds United
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewatolea
wito wachezaji kama vile Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard,
wote wakiwa na umri wa miaka 25, kupunguza mapumziko yao ili
kuwasaidia wachezaji katika timu zao wenye uwezo mdogo ambao wameshindwa
kufanikiwa kucheza mchezo wa kuridhisha katika kipindi cha kabla ya
msimu (Times - subscription required)
Mchezaji wa England
anayeichezea kikosi cha Middlesbrough cha vijana walio chini ya miaka 21
kwa sasa Patrick Bamford, mwenye umri wa miaka 24, yuko karibu kuhamia
kwa mahasimu wao katika Ligi ya Championi Leeds United kwa gharama ya
awali ya awali ya kanda ya £7m. (Guardian)
Wakati huo huo , Boro
wamekataa pendekezo la Wolves ambao ni wageni katika Premier League
ya kumchukua winga wao Adama Traore mwenye umri wa miaka 22 . (Express
& Star)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Mlinzi wa Everton Matty Pennington (kulia) analengwa na Leeds kwa ajili ya msimu ujao
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Morocco Younes
Belhanda, anayeichezea Crystal Palace, amemua kuwa hatahamia England na
kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 anasisitiza kuwa anafurahia kuwa
Galatasary Turkish. (Football.London)
Mchezaji wa safu ya kati wa
Paris St-Germain Mfaransa Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 23,
anakaribia kusaini mkataba na Ligue 1 champions. (ESPN)
Mlinzi
wa Everton Matty Pennington analengwa na Leeds - ambako alikuwa katika
msimu uliopita kwa deni na Wigan pia wanamtaka Muingereza huyo mwenye
umri wa miaka 23.. (Liverpool Echo)
Kocha wa zamani wa walinda
lango Kevin Hitchcock ameteuliwa kufanya kazi hiyo hiyo katika timu ya
Super Ligi ya India ya Chennaiyin FC -akijiunga na meneja wa zamani wa
Aston Villa John Gregory. (Birmingham Mail
Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.
0 maoni:
0758057161