
Unaonekana uhusiano wa wapenzi
maarufu Afrika Mashariki yaani msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz
na mfanya biashara wa Uganda Zari Hassan umefika ukingoni.
Zari
Hassan ametangaza kuachana na mzazi mwenzake, Naseeb Abdul maarufu
Diamond Platinumz baada ya kuwapo kwa tuhuma nyingi kuhusu mwanamuziki
huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine. Mashabiki wa Zari wamepokea habari hizo kwa mshangao na hisia tofauti wakituma ujumbe kwenye ukurasa wake.



Tangu hilo litokee mambo hayajakuwa shwari kati ya hao wawili.
Zari ametangaza uamuzi wa kuachana na Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema baada ya tuhuma nyingi dhidi ya mpenzi wake kuwa na wanawake wengine kila mara ameamua kuulinda utu wake na kuachana naye.
0 maoni:
0758057161