Ubalozi wa Marekani Tanzania unataka uchunguzi baada ya kifo cha mjumbe wa upinzani
Ubalozi wa Marekani Tanzania unataka
uchunguzi huru kuhusu matukio ya matumuizi ya nguvu dhidi ya harakati
za kisiasa za upinzani.
Hii ni baada ya kifo cha mjumbe wa chama
cha upinzani CHADEMA, Daniel John tarehe 11 Februari, ambaye mwili wake
ulipatikana katika fukwe za bahari ya hindi, jijini Dar es salaam, siku
moja baada ya kutekwa ukiwa na majeraha ikiwemo shingo yake kunyongwa
na watu ambao hadi saa hawajajulikana.Marehemu anaripotiwa kutekwa pamoja na mwenzake, Reginald Mallya aliyenusurika na kupatikana akiwa hai akiwa na majeraha kadhaa sehemu za mkononi na kichwani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa balozi wa Marekani, balozi wamesema "Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu."
"Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana."
Pamoja na hayo ubalozi umetaka "uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania."
Tukio hilo limefayika ikiwa ni juma la mwisho la kampeni za uchaguzi mdogo katika majimbo mawili nchini Tanzania ambayo yalipoteza wabunge wake kwa sababu mbalimbali ikiwemo ile ya wabunge wa upinzani kujiuzulu kwa kile walichokiita kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano.
Kwa upande wake, kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Murilo, amesema polisi waachwe wafanye uchunguzi kufuatia vitendo hivyo vya utekaji nyara.

0 maoni:
0758057161