
Kutoka rais Truman hadi kufikia kwa
Trump, Marais wa Marekani wamekuwa na mahandaki ya kukwepa mashambulio
ya kinyuklia. Hivyobasi ni nini kinachofanyika iwapo kuna tisho la
kinyuklia.
Mara moja rais Trump atatoroshwa katika eneo lenye usalama, ana maeneo mengi ya kumficha .Mojawapo lipo ndani ya ikuku ya Whitehouse, handaki lililojengwa miaka 1950.
Eneo jingine liko chini ya ardhi katika eneo la Blue Ridge Mountains huko Virginia.
Pia ana handaki jingine katika nyumba yake mjini Florida na jingine ambalo hutumiwa kuhifadhi mabomu katika uwanja wake wa kucheza gofu katika eneo la West Palm Beach.
Handaki hilo linadaiwa kuwa chini ya shimo la pili katika uwanja huoHabari ya kumlinda Trump ,iwapo kutakuwa na shambulio la bomu. inaonyesha vile Wamarekani wamekuwa walikijadili swala la kutokea kwa vita vya kinyuklia katika kipindi cha miongo kadhaa iliopita.
Kwa wengine , wazo la kuzuka kwa vita vya kinyuklia halipo katika mafikira yao. Wengine wanajiandaa.

Hathivyo hakuna handaki linaloweza kuhimili shambulio la moja kwa moja. Iwapo rais ataipuka shambulio la kwanza atalazimika kupelekwa mahali ambapo atalazimika kuliongoza taifa, hata iwapo ulimwengu uliosalia upo katika vita.
Maafisa wa Marekani wamefanya maandalizi ya rais na kundi la maafisa wa ngazi za juu serikalini , kulingana na Robert Darling ,mwanamaji aliyehudumu kipindi cha Septemba kumi na moja katika handaki la Ikulu ya Whitehouse.
Ametaja ni akina nani walioruhusiwa kuingia ndani.
Kama alivyosema Darling. Ni watu wachache pekee walioruhusiwa kuingia katika handaki la rais .
Ujenzi wa nyumba na mahandaki aidha ya marais ama raia wa kawaida una sababu yake-unafanya kuwa rahisi kwa raia wa Marekani kuzungumzia kuhusu maswala ya Atomic ama ya kinyuklia na kufanya wasio fikiriwa vita vya kinyuklia dunia kufikiria.
Harry Truman alianzisha utawala wa kiraia wa ulinzi 1950.
Ujumbe wa jumla kutoka kwa serikali ni kwamba , kulingana na Christian Appy ,muhadhiri wa somo la historia katika chuo kikuu cha Massachussets mjini Amherst, ni kwamba vita vya kinyuklia sio lazima viangamize kila mtu.
0 maoni:
0758057161