Thursday, 16 November 2017

Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'

Posted at  November 16, 2017  |  in  

Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia)Mugabe (wa pili kulia) akiwa kuzuizi cha nyumbani akisimama na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga (kulia) 
 Rais wa miaka mingi nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.
Mugabe, 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema.
Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake
Robert Mugabe alikutana na mkuu wa majeshi aliyeongoza hatua dhidi yake
 Jeshi lilichukua hatua baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa, wiki iliyopiya, na kuashiria kuwa alimpendelea mke wake Grace Mugabe, kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF na kuwa rais.
Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa Bw. Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.
Maafisa wa Zanu PF mapema walikuwa wamesema kuwa Bw. Mugabe atasalia madarakani hadi ufanyika mkutano mkuu wa Chama mwezi Disemba wakati Bw. Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa raisBw Mugabe alikutana na maafisa katika ikulu ya HarareBw Mugabe alikutana na maafisa katika ikulu ya Harare

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 maoni:

0758057161

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 UKWELI ZAIDI.
Powered by Themes24x7 .
back to top