Thursday, 16 November 2017

Kampuni ya Uswisi yafungua kiwanda cha kemikali Tanzania

Posted at  November 16, 2017  |  in  

Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli
Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli 
 Kampuni kutoka nchini Uswisi imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari.
Florence Tinguely Mattli ni balozi wa Uswisi nchini Tanzania, ameiambia BBC kuwa suala la uwekezaji ni hatua ya kujiamini kwanza na kutoona hasara.
Alipoulizwa kuhusiana na sera za uwekezaji nchini Tanzania kudaiwa kuwa si rafiki Bi.Mattli amesisitiza kuwa uzoefu wao kiviwanda na kuwekeza katika mataifa mbalimbali duniani itawasaidia kujua ni mambo gani ya kuzingatiwa katika uwekezaji wao Tanzania katika serikali ya awamu ya sasa.Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja
Kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja
 Waziri wa viwanda wa Tanzania Dr Charles Mwijage anasema kuwa dira ya mwaka 2025 ni kuhusiana na viwanja.
Meneja mkuu wa kiwanda hiki cha Kemikali cha Sika Tanzania Alfonso Paradinas anasema kiwanda chake kitazalisha kemikali hizo za ujenzi na kuongeza ubora wa majengo nchini humo.
Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa kanda ya Sika ya Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika Ivo Schaedler lengo lao ni kutumia soko la Tanzania na kuongeza ufanisi nchini humo,na kuongeza kuwa wana viwanda 17 ndani ya Afrika.

Share this post

About Naveed Iqbal

Nulla sagittis convallis arcu. Sed sed nunc. Curabitur consequat. Quisque metus enim venenatis fermentum mollis. Duis vulputate elit in elit. Follow him on Google+.

0 maoni:

0758057161

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 UKWELI ZAIDI.
Powered by Themes24x7 .
back to top